Posts

Showing posts from August, 2025

262. BADO KITAMBO

Bado kitambo - vita itakwisha, Kitambo Na dhoruba zapoa. Na tena nitalaza kichwa changu Mbavuni mwake Anipendaye. :/:Mbinguni hazitakuwamo Dhambi, Nitaziona raha na amani.:/: Bado kitambo - roho ya umizwa, Kitambo, Kati' usiku huu. Machozi ninatoa mara Nyingi, Maana bado sijamwona Yesu. :/: Lakini asubuhi ya milele, Huko Mbinguni sitalia tena.:/: Bado kitambo cha uchovu huku, Kitambo na nitamwona Yesu, Na huru Mbali ya hatari zote, Nastarehe mikononi mwake. :/: Uvuli wote utaondolewa, Kwa Nuru huko kamilifu kweli.:/: Mateso yangu hayadhuru tena, Nitayasahau kwake Yesu, Nikisumbuka Hapa duniani, Mbinguni nitastarehe  Kweli. :/: Na Mungu atafuta kila chozi, Ataondoa maumivu yote.:/:

263. ENYI KANISA LA MUNGU

Enyi kanisa la Mungu Punde vumilieni! Kati' nchi ya milele, Mtaona amani. :/: Kitambo kidogo, Na vita itakwisha.:/: Usilogwe na dunia, Usiache wokovu! Katika shida na raha, Umfuate Yesu tu! :/: Daima, daima, Utashida ubaya.:/: Ukichoka safarini, Njia ikiwa ndefu, Kwa hatari za jangwani, Mungu atakulinda. :/: Raha ya mbinguni, Yamtuliza msafiri!:/: Kwa imani tutaona Nchi yetu ya raha, Ni habari nzuri sana: Majaribu yakoma. :/:Twendeni, twendeni, Tukutane mbinguni!:/: Tukifariki dunia, Kwa furaha twaenda, Tulivyovitumaini, Ng'ambo tutaviona. :/: Furaha, furaha, Furaha ya milele.:/:

264. TWENDENI, WAKRISTO

Twendeni Wakristo wam-pendao Yesu, Tumwimbie na furaha, Tumwimbie  na furaha Kitini kwa Mungu, kitini kwa Mungu. Twendeni  mbinguni sisi tuliookoka, Twendeni tukatazame fahari ya Bwana wetu. Hawatafurahi wasiomjua Yesu, Bali tuokolewao, bali tuokolewao, Tum-sifu pote, tum-sifu pote. Tuna mibaraka yake, Mwokozi tele, Kabla hatujafikia, kabla hatujafikia Mji  wake Mungu, mji wake Mungu. Kwa hiyo twendeni furaha izidi, Tuache huzuni zote, tuache huzuni zote, Tufike kwa Yesu, tufike kwa Yesu.

265. TU WASAFIRI

Tu wasafiri, twakaribia Nchi ya Mbingukwa Mungu, Tusiogope bonde la kifo, Yesu anatuongoza. :/: Tu wasafiri :/: Tutakutana kwa Baba Mungu, Ee Bwana Yesu, utuongoze, Tufike sote Mbinguni. Wengi katika wapendwa wetu, Wamevuka mto wa kifo. Walifuata wito wa Mungu, Wakahamia huko juu. Katika mwendo wa duniani, Walimtazama Mwokozi. Na waliacha mambo ya huku, Walimpendeza  Yesu. Ndugu wapendwa, tuendelee, hata Tukiwa na shida! Yesu ni njia, kweli, Uzima, Tumfuate daima!

266. NATAKA NIMJUE YESU

Nataka nimjue Yesu, Na nizidi kumfahamu, Nijue pendo lake na Wokovu wake kamili. Zaidi, zaidi, nimfahamu Yesu, Nijue pendo lake na Wokovu wake kamili. Nataka nione Yesu, Na nizidi kusikia, Anenapo kitabuni, Kujidhihirisha kwangu. Nataka nifahamu na, Nizidi kupambanua, Mapenzi yake nifanye, Yale yanayompendeza. Nataka nikae naye, Kwa mazungumzo zaidi, Nizidi kuwaonyesha, Wengine wokovu wake.

267. BABA NAKUOMBA

Baba, nakuomba asubuhi hii, Niongoze kweli katika yote. Ee, Baba sikia Maombi yangu. Nakusifu Baba, Wanisikia. Ninapoifanya kazi ya leo, Unitie nguvu, naomba Bwana. Mchana uishapo, usiku waja, Baba unilinde, ninakuomba. Maadui wengi wananiwinda, Maishani mwangu. Mungu 'nilinde! Siku zangu zote ulimwenguni, Niwe na amani, hadi mwishoni.

268. EE YESU INGIA ROHONI

  Ee Yesu ingia rohoni mwangu, Ili nitakaswe Niwekwe huru, Nipate kushirikiana  nawe, Katika mateso na raha yako. Nifahamishe uwezo wako!  Nisulubishwe pamoja nawe! Nifahamishe  uwezo wako! Nisulubishwe pamoja nawe! Siombi ufalme, siombi sifa, Naomba neema Yako daima, Nijue yakini ya msalaba, Ulipokufa Kwa ajili yangu. Ingia rohoni, unichunguze, Unisaidie katika Yote, Kusudi nipate nia moyoni, Nijitoe kweli Kwako Mwokozi. Hakuna neno la kunizuia, Kuwa na umoja Nawe Mwokozi, Nitawezaje kufika mbinguni, Nisipounganishwa naye Yesu?

269. ENENDENI ULIMWENGUNI

Enendeni ulimwenguni, Milimani Hata mabondeni Kuihubiri  Injili, Msifuni Bwana Yesu! Msifuni Yesu! Msifuni Yesu! Tangazeni Neno lake! Msifuni Bwana Yesu! Mchana hata usiku, Eneza Neno la Bwana Yesu, Nuru inapotokea, Msifu Bwana Yesu! Na kama vile malaika, Wanavyomhimidi Mwokozi, Nasi tumwimbie hivyo, Tumsifu Bwana Yesu! Mwenzangu kabla hujaitwa, Kuondoka Hapa duniani, Ujisafishe damuni! M-sifuni Bwana Yesu!

270. SIMAMA FANYA VITA

Simama fanya vita, askari wa Yesu! Tuinue bendera ya ushindi wake! Yeye huyaongoza, majeshi yake huku, Adui wote pia, Bwana awashinda. Sikia baragumu, linalotuita! Tuendelee mbele, Lengo ni kushinda! Tusiogope  kamwe, hatari za vitani, Pigana na adui, kwa nguvu za Mungu! Simama fanya vita, kwa jina la Yesu! Yafaa sisi sote, kumtegemea. Na kwanza tuzivae, Silaha za Mungu! Tukeshe siku zote, tuombe kwa bidii! Shindano letu hapa, hima litakwisha, Ndipo tutapumzika, baada ya vita. Na kila mshindaji, atapokea taji, Na utukufu mwingi, Karibu na Mungu.

271. NINASHIKWA NA KIU

Ninashikwa na kiu, Bwana, unipe maji, maji ya uhai ndani ya maisha yangu. :/: Bwana, Bwana Yesu Mfalme wangu!:/: Moyo wangu wakupenda, Bwana Mungu wangu. Nitakuja lini kwako, Bwana Mfalme wangu? Mchana na usiku Bwana nakulilia. Watu Wasema "Mungu wako yuko wap?" Huzuni moyoni mwangu, Bwana Mungu wangu. Watu wengi  wadharau, Mungu 'wasamehe! Twashikakama pamoja kwenda juu mbinguni. Twashukuru, twafurahi kushirikiana. Mwokozi, nguvu zaishaje moyoni mwangu? Unisaidie Bwana, nitakushukuru.

272. NI SIKU TUKUFU

Ni siku tukufu, haleluya amina, Ya kupum-zika, haleluya, amina. Tuache shughuli tumwabudu Mungu, Bwana wa mbinguni, haleluya amina. Ni siku tukufu, haleluya amina, Tukufu kabisa, haleluya, amina. Njoni ndugu zangu, tumwabudu Mungu, Kwa roho na kweli, haleluya, amina. Ni siku tukufu, haleluya, amina, Ya furaha mno, haleluya, amina. Yesu 'kafufuka, na sasa yu hai, Anatuombea, haleluya, amina. Ni siku tukufu, haleluya, amina, Ndiyo maarufu, haleluya, amina. Tunaye Mwokozi atuokoaye, Sasa na milele haleluya, amina. Ni siku tukufu, haleluya, amina, Siku ya neema, haleluya, amina. Tangazeni Neno la Bwana Mwokozi, Msifuni daima, haleluya, amina.

273. NI UHERI KUMWAMINI MUNGU

Ni uheri kumwamini Mungu, Kama Ibrahimu  zamani. Hakutiwa shaka  kwa uchungu, Ila alitiii kwa imani. Ni uheri kuendea sawa, Katika mapito ya kweli. Ukijaribiwa na kukawa, Mwisho wake utajaliwa. Mashujaa wote wa Biblia, Hawakufuata anasa. Wakafunzwa kum-tegemea, Mungu Baba mwenye uweza Nao wakaenda kwa imani, Ya kutetemesha dunia Wkashida giza na shetani, Sifa na heshima kwa Mungu. Yeye atakayekuzwa naye Kwanza, atajinyenyekeza. Baba anayempenda Mwana, Anamrudi kwa upendo. Hivyo Mungu anawakamilisha watu wake wanapoteswa. Na zaidi kuwafahamisha kulijua pendo lake kuu. Na ikiwa raha ya dunia yatoweka kwa majaribu. Mwaminifu atamfurahia Mungu kwani yupo karibu. Na mavuno ya taabu yake Yakitekelezwa motoni, Atamgemea Bwana wake, Kwa  hiyo hatanung'unika. Jipe moyo enyi kundi dogo msiogope hatarini. Shika neno la Mwenyezi Mungu liwaongoze safarini. Haleluya kwani majaribu yanahimiza msafiri. Naye ataona kwa karibu Mji wa amani Mbinguni.

274. NAFURAHIA KISIMA DAIMA

Nafurahia kisima daima Cha damu ya Yesu Kristo Katika upendo nalindwa vema, Namsifu Yesu mpendwa. Chemchemi hiyo inabubujika, Yaniletea uzima Kando ya maji ninaburudika, Nashangilia daima. Nakaa karibu na kisima hiki, Naishi kwa maji yake. Yaniletea  kupita kipimo, Uzima na shangwe kweli. Nakaa karibu na kisima hiki, Naishi salama sana. Fika upesi uliye na kiu, Kisima chabubujika! Nakaa karibu na kisima hiki, Ni furaha na uheri. Na kando ya maji nafasi ipo, Waweza kupona kweli.

275. EE MUNGU MWENYE HAKI

Ee Mungu mwenye haki, niongoze huku Katika mambo yote yakupendezayo. Bila wewe, Bwana Yesu, mashaka mengi ninayo Ya kunitisha hapa safarini mwangu. Kumtegemea Yesu ni heri daima, na kutembea naye kwa kila hatua, Kwa kuwa yeye ni Mchunga. Ananiongoza vema, Nipate kuingia kwake mbinguni juu. Nina safari sasa ya kwenda mbinguni. Mwokozi yuko huko, Lazima nifike. Na siku ya kuingia Nitashangilia kweli Kumwona na kum-sifu Mwokozi wangu. Ulimwenguni huku kuna shida nyingi, Nikihitaji kitu, ninahangaika. Lakini siku ile kuu nitakapomwona Yesu, Natumiani  sitaikosa Thawabu. Mbinguni sitaona uovu wowote. Wala kukuta Mambo ya huzuni tena. Sauti nitamtolea kusema: "Ee, Mungu mwema!" Mikono nitaipepea kwa shangwe kuu.

276. EE MUNGU MWENYEZI

Ee Mungu Mwenyezi, matendo yako Yapita fahamu zote, lakini hakika najua kwamba, Njia yako ndiyo bora. "Mtoto wangu huwezi kujua, Jinsi nikutendeavyo. Lakini usiogope mwanangu, Mateso yote 'takwisha." Ee Bwana, unayo magari mengi Na lile linalonifaa, Unichagulie mwenyewe, Bwana, Nifike salama kwako! Na kama nitaondoka haraka, Kama Eliya zamani, Uchungu na shida zote 'takwisha, Nitakwenda kwa amani. Tutamsujudia Yesu pamoja, Na watakatifu wote. Mungu mwenye haki hata milele, Katika matendo yake. Nangoja kwa uvumilivu sasa, Kuchukuliwa na wewe. Natarajia uzima milele, Uridhi wangu mbinguni.

277. NITAKAPOTOKA DUNIANI

  Nitakapotoka duniani, Na kusimama mbele za Mungu, Nitamwona Mkombozi wangu, Itakuwa utukufu kweli. Itakuwa utukufu, utukufu, utukufu, Kumwona Yesu Mwokozi wangu. Itakuwa utukufu kweli. Huko mbinguni nitakapokaa, Pamoja nao watakatifu, Nitamshukuru Mwokozi wangu, Itakuwa utukufu kweli. Nitawaona wenzangu wote, Waliozishinda dhambi zote. Na nitamwona Mwokozi wangu, Itakuwa utukufu kweli. Je, ndugu umejitayarisha Kumwona Yesu Mwokozi wako, Ili na wewe ushangilie, Na kuona utukufu kweli?

278. NINAINUA MACHO YANGU.

Ninainua macho yangu Kwa Mungu aketiye juu, Aliye msaada wangu, Njiani mwangu ni nuru, Aliyefanya yote, Husikia maombi. Katika njia Yangu yote Anilinda vema kweli. Bwana hataniacha kamwe miguu yangu iteleze, Yeye ndiye Mlinzi mwema, Ambaye hatasinzia. Alinda roho yangu, Nisije kupotea, Baraka zake Zinatosha, Kwa hitaji zangu zote. Aniokoa na uovu, Aniponya roho yangu. Yeye ni nguvu na wokovu, Ninahakikisha kweli. Ananilinda pote, Kutoka na kuingia. Anijalia mema yote, Nikimtumainia.

279. MWOKOZI ALIFUFUKA

Mwokozi alifufuka, Haleluya! Watu wote mwimbieni, Haleluya! Imbeni kwa furaha, Haleluya! Viumbe vyake vyo vyote, Haleluya! Kristo alituokoa, Haleluya! Akamshinda Shetani, Haleluya! 'Katuokoa gizani, Haleluya! Kutuingiza nuruni, Haleluya! Makaburi mengi sana, Haleluya! Yakafunuka kabisa, Haleluya! Ikashindwa mauti, Haleluya! Kristo ndiye M-shindaji, Haleluya! Mfalme yu hai mbinguni, Haleluya! Alitushindisha kufa, Haleluya! Alileta uzima, Haleluya! Akaondoa hukumu, Haleluya! Yesu ana utukufu, Haleluya! Nasi tutaishi naye, Haleluya! Tutakapofufuka, Haleluya! Tutafanana na Yesu, Haleluya! M-falme wa ulimwengu, Haleluya! Njoni tumhimidi sote, Haleluya! Tumwabudu Mwokozi, Haleluya! Ndiye ufufuo wetu, Haleluya!

280. JINA LAKE YESU KRISTO

Jina lake Yesu Kristo Lina nguvu daima. Jina hilo la ajabu litadumu milele. Linafaa kwa watu wote, wazee na vijana. Linaweza kuongoza Kila  mtu kwa Mungu. Jina hilo nalipenda, Lawasha moyo wangu, Na kwa jina hilo jema, Nimepata wokovu. Jina hilo linavuma Po pote duniani, Na kwa wote linaleta, Raha na tumaini, Jina hilo laondoa machukio moyoni, Ndipo milki ya Mwokozi, Itapata nafasi. Na katika giza huku, Jina hilo linang'aa, Laonyesha msafiri, Njia yenye uzima. Jua likitiwa giza, Jina hilo ladumu, Na milele lisifiwe, Hapa na mbinguni juu.

281. YOTE NINAYO NI KWA NEEMA

Yote ninayo ni kwa neema, Tangu Nilipomwamini Bwana, Dhambi  na hatia Zikafutwa, kwa neema yake nimeokoka. Ameniokoa, Mwokozi Niliyekuwa mwenye Dhambi, Niliyekufa nimefufuliwa, Kwa neema yake nimeokoka! Nilitawaliwa na Shetani, Kuelekezwa Upotevuni, Bali Yesu akanitafuta, Kwa neema yake nimeokoka. Natakaswa na Yesu Mwokozi, Si kwa Majuto wala machozi, Bali kwa damu Nakombolewa, Kwa neema yake nimeokoka Nimejaa shangwe na furaha, Na ninaimba Nashangilia,  Kwa kuwa amenirehemia Kwa neema yake nimeokoka.

282. UKIHITAJI KWELI UTUKUFU

Ukinihitaji kweli utukufu wa Bwana, Ujalivu wa Roho, Shika Neno la ahadi na umwendee Baba kwa njia ya Imani! Atajaza moyo wako ufurike. Bwana Yesu aita, Njoo bila kusita! Atajaza moyo wako afurike Roho Mtakatifu. Vichukue vyombo vyako, Vioshe viwe safi Kisimani Golgotha. Ujitoe kabisa kwa Baba na utapewa, Roho moyoni mwako. Mafuta hububujika hayakomi kabisa, Kadhalika upendo. Anataka kukujaza na Roho wa ahadi, Mpokee kwa imani!

283. NIMEYASIKIA MENGI

Nimeyasikia mengi aliyofanya Yesu Alipokuwa hapa duniani. Pote alienda mema, aliwasaidia. Kwa furaha ninaimba: "Yesu ni yeye Yule." Yesu ni Yeye  Yule Jana leo, daima! Hutafuta wakosa, Huokoa waovu. Mwokozi ni yeye Yule Ni kipofu yule, Jina lake ni Bartimayo, Aliposikia Yesu apita, Kwa imani akaomba Akaponywa na Yesu. Nafurahi kwa kuimba: "Yesu ni yeye Yule". Wenye dhambi na wagonjwa na maskini waitwa kwa Yesu, Mwokozi mwenye rehema. Uiguse nguo yake, sawa na mama yule, Utapewa nguvu zake, Yesu ni yeye Yule! Najisikia jinsi alivyowaombea Maadui wake msalabani. Aliteswa kwa miiba, aliona uchungu. Kwa furaha ninaimba: "Yesu ni yeye Yule".

284. TUMESOMA MENGI

Tumesoma mengi juu ya Bwana Yesu Upendo wake, ishara zake. Na usome tena, Ukamwombe Mungu, Na utaona maajabu. Hata leo yanatokea, Tunapoomba kwa imani. Tuombe tu, Atusikia, Na tuatona maajabu. Jamaa ya Naini wakosa amani, Wafadhaika, Wahuzunika. Bali Bwana Yesu 'kafanya ajabu. Aliyekufa 'kahuika. Ahadi ya Mungu, Roho mtakatifu, Ilitimizwa Yerusalemu. Walikutanika, Roho akashuka, Kwa lugha mpya wakamsifu. Petro kahutubu, wengi wakatubu, wakagairi Dhambi za siri, Waliopokea Neno lake Bwana Wakabatizwa siku ile. Nilimwomba Yesu, Nikapata nguvu, Na jambo hili ni la fadhili, Nilisamehewa Dhambi zikafutwa, Nimeupokea wokovu.

285. SOMA BIBLIA

  Soma Biblia, chuo cha wokovu, Tulichopewa na Mungu Baba. Biblia inatuambia kweli: Njoo kwa Yesu Mwokozi wetu! Chunguza neno tulilopewa, Linatuonyesha njia ya kweli, Nuru gizani ya kutuongoza Katika mwendo kwenda Mbinguni. Soma Biblia, giza linakuja Kama walivyosema manabii. Biblia yetu yatuangazia Kutuonya  njia hata mwisho. Katika neno la Biblia yetu Tunapewa utajiri wote. Mbingu na nchi zitaangamia, Neno la Mungu halitapita.

286. ARUSINI HUKO KANA

Arusini huko Kana Yesu alialikwa, Hapo ikaonekana Ishara ya ajabu. Ushushe Baraka zako Ju-u ya ndugu hawa, Bana na Bibi -arusi. Uwaongoze vema. Leo tunakuhitaji Uwe pamoja nao, Bwana na Bibi-arusi. Ndoa ibarikiwe Yesu U mlinzi wao, Uwalinde taabuni. Uhifadhi nyumba yao, Waishi kwa imani. Katika raha na taabu Wafungane kwa pendo, Watumike kwa Furaha Mpaka siku ya mwisho.

287. MUNGU BABA WA MBINGUNI

Mungu Baba wa mbinguni Usikie maombi, Ndoa hii uibariki Idumu kwa imani. :/:Ee Mungu, bariki Ndugu hawa wawili:/: Ndugu hawa mbele zako Na mbele ya Kanisa watimize Neno lako, Wapendane daima. Ndugu wawe na umoja Kwa shida na furaha, Kama Yesu na Kanisa Wanavyounganika. Bwana walinde daima, Bariki nyumba yao, Ili waishi salama, Kwa raha na upendo. Wabariki, Mungu Baba, Watu hawa wawili, Wape upaji wa wana, Wafurahishwe kweli. Siku zao duniani Zitakapotimia, Wape urithi mbinguni, Pamoja naye Yesu.

288. TUNAMTIA MIKONONI MWAKO

Tunamtia mikononi mwako Mtoto huyu ili, Atunzwe, Na kila siku kwa neema yako, Bwana Yesu Kristo, umbariki! Ulimwengu kuna majaribu, mahali Pote kuna mitego, Lakini uwe Mchungaji wake, Na umwongoze, Ee Rafiki Mwema. Yesu umhifadhi kwa upendo, Asije Akashindwa njiani, Na umlinde kwa Rehema yako, Apate kuwa wako siku zote. Utume nuru ya neema kwako, Na maji Hai kutoka kwako, Ee Bwana Yesu Twaku-omba leo: "Umlinde mwana wetu Salama!"

289. NINATAMANI KWENDA.

Ninatamani kwenda mbinguni nchi yangu, Niliyepewa na Mungu kwa imani. Ni Shangwe bora kuona mji ule, Kwa Kwenda kule sitaogopa kitu. Ee Baba yangu niongoze, unisafishe  kwa damu ya Mwokozi! Nifananishe na theluji, Unibatize kwa Roho Mtakatifu! Ee Mungu tumepata Mwana Yesu Kristo. Kipawa kweli kinachoshinda yote. Anahubiri amani kwao wote, walio huku Kribu, nao mbali. Kwa Yesu tumepata mwisho wa upendo Na njia ya kumwendea Baba Mungu. Si Wapitaji na tena si wageni, Tunatumika Kwa roho ya upendo. Amani kwetu na matumaini tele, Salamu Toka kwa Mungu wa milele. Ni posho ya Watumishi wa upendo Tutaurithi uzima Wa milele.

290. BARAGUMU LITALIA SANA

  Baragumu litalia sana, Watu wote Watalisikia. Waliokufa watafufuka na Wazima watabadilika. :/:Nani anayeweza? Yesu mwenyewe uwezo:/: Na wenye uwezo wa duniani Watatetemeka  siku ile. Na hawataweza kuinuka Kutazama uso kama jua. :/: Nani anayeweza? Yesu mwenye uwezo:/: Najua Mchunga wangu mwema, Anichunga Kwa maisha yangu,  Na siku ile ya mwisho nikishinda, Sitaona uchungu wa kufa. :/:Nani Mchunga mwema? Yesu Mwenye uwezo:/: Mbinguni hakitafika kitu cha uchafu, Dhambi na kuasi. Wasiomwamini Bwana Yesu Ghadhabu  ya Mungu yawangoja. :/: Nani atahukumu? Yesu mwenye uwezo:/: "Mimi Yesu mzabibu wa kweli, Baba Mungu Ndiye mkulima, Na ninyi matawi ndani Yangu, Na hamwezi neno bila mimi." :/: Nani ni mzabibu? Yesu mwenye uwezo.:/: Unayempenda  Baba Mungu lazima Umpende ndugu yako, Ukiwa hupendi ndugu yako, Huwezi kumpenda Baba Mungu. :/: Nani aliyesema? Yesu Mwenye uwezo.:/: "Nawapenda mwisho wa Upendo, Na ninyi Mpate kupendana, Hivyo mataifa Wataona ya kwamba m-watu w...

291. MIMI MKOSAJI NILIKOMBOLEWA

Mimi mkosaji nilikombolewa, Alipojitoa Mwokozi. Dhambi zangu zote Alizichukua, Kwa damu nilikombolewa. Dhambi zilitungikwa msalabani, Alipojitoa Mwokozi. Maumivu makuu! Walimdharau, Alipobeba dhambi zangu. Yesu wa upole anihurumia, Ananitakasa Rohoni. Nimesafishwa na nimewekwa Huru toka laana ya torati. Naambatana na Yesu, siondoki, Kwa Kuwa alinificha. Yesu, nakusifu Uliyepenipenda, Ukachukua dhambi zangu.

292. KATIKA DAMU

Katika damu safi ya Yesu Dhambi zangu Zilifutwa. Katika mto ule wa afya Nalindwa na nguvu zake. Nguvu za wokovu!  Nguvu za ushindi! Nazipata kisimani kinachojaa tele. Nguvu za wokovu! Nguvu za ushindi Damu inayonisafisha. Kwa wingi wa neema ya Yesu Nimepona, Nimepona! Wokovu ni kwa ajili yako, Na Kwa kila 'aminiye. Nguvu zangu hazitoshi kweli, Ni dhaifu, Ni dhaifu, Ila Yesu anifahamuye, Aniwezesha daima. Baba yangu mwema anipenda, Anipenda, Anilinda! Sitaogopa nguvu za mwovu, Yesu yu pamoja nami.

293. NCHI NZURI YA RAHA

Nchi nzuri ya raha kweli kwa hamu Twaitazamia. Yesu atungojea huko, Ametayarisha makao. Kitambo kidogo tuonane mbinguni huko! Kitambo kidogo tuonane mbinguni huko! Huko kuna amani tele, Tutashangilia Milele, Tutamsifu Mwokozi wetu, Sababu alitufilia. Baba Mungu atupendaye, Kwake kuna Furaha nyingi. Twamsifu kwa neema  Yake, Inayotutosha milele.

294. UTUME ROHO WAKO

Utume roho wako juu yetu Kama kwa Siku ya Pentekoste. :/: Uwashe moto wako Ndani yetu, Tusiwe wenye uvuguvugu.:/: Utume Roho wako juu yetu Kama Ulivyofanya zamani, :/: Mtume Petro Alihubiri katika nyumba ya Kornelio,:/: Utume Roho wako juu yetu, Tupewe nasi Uwezo wako.:/: Maelfu wenye dhambi Waokoke na Neno lako tulieneze.:/: Utume Roho wako juu yetu, Nyosha Mkono wako wa nguvu, :/: Ishara na ajabu Zifanyike wagonjwa waponywe kati yetu.:/: Uwaamshe waliosinzia, Waliodhoofika Safarini. :/: Ee Bwana, utujie kama kale Ulipowapa watu Baraka.

295. SHANGILIENI EE WATU WA MUNGU

Shangilieni Ee watu wa Mungu! Yesu Bwana alitumwa kwetu. Neema kubwa, Pendo la ajabu tum-sifu Mungu siku zote! Mungu wetu mwenye mamlaka yote U ngao na kimbilio letu, Unayasikia maombi yetu, jina lako litukuzwe! Shangilieni Ee watu wa Mungu! Tumwimbie nyimbo za furaha! Tusiogope Bali tumwamini, Twende mbele kwa uwezo Wake! Shangilieni Ee watu wa Mungu! Tumeokoka kutoka dhambi. Jirani zetu Wasioamini, tuwaongoze wamjue Yesu! Shangilieni Ee watu wa Mungu! Mfalme Wetu yuaja tena! Kitambo kidogo tutaingia Mbinguni kwake Mwokozi wetu!

296. DHAMBI ZANGU ZIMEONDOLEWA

Dhambi zangu zimeondolewa, Mambo ya Giza nimeyaacha. Yesu Kristo amenisafisha, Ninamfurahia Mwokozi wangu. Ninalo kao mbinguni Nami nimepewa vazi, Thawabu ya ushindi ni Taji ya uzima. Yesu ni Mwokozi wangu. Alinikomboa, Alilipa deni langu Pendo lake kubwa nalisifu daima, Ninamfurahisha Mkombozi. Nimeokoka toka gizani, Zimekwisha siku Za huzuni. Nikitapa raha na amani, Wakati Yesu aliponikomboa. Shaka na hofu zimeondoka, Na siogopi Mauti tena.  Yesu Kristo ni rafiki yangu. Kwake ninalindwa vema siku zote. Roho wa Mungu anijaliza, Ananifariji Safarini. Yesu Kristo yu karibu nami, Yeye ni ngao yangu  na kimbilio.

297. CHAKULA CHA ROHO

Chakula cha roho Nipe Bwana, Ulivyogawanya mkate kale. Bwana wangu nakutegema. Kwa neno uonekane kwangu. Ukaja mkate Wa uzima. Ni neno linaloniokoa. Nipe nguvu  zako, na daima Nigawie Neno la uzima. Bwana umtume Roho wako Kuniongoza katika Neno. Uniguse macho, niwezeshe Kukutazama katika Neno.

298. NINAO WIMBO

Ninao wimbo wa kunifurahisha Wa Mwokozi, Wa Mwokozi. Namshukuru Kwa moyo na kwa roho Mwokozi mzuri mno. Mwokozi-wimbo wangu, Ni Yesu, Ni Yesu! mahali pote na siku zote nitamsifu Yesu kwa yote. Mwokozi -wimbo wangu huku na mbinguni. Jina lake lafanana na marhamu, Jina lake Ndilo Yesu. Kutoka kwake Napata vita Vyema, Mwokozi mpendwa wangu.

299. UNAJUA JINA TULILOPEWA

Unajua jina tulilopewa tuokolewa kwalo? Linasifiwa duniani pote katika watu wote. Yesu ndilo jina lipitalo Kila jina duniani! Ni lenye nguvu ya kutuokoa kutoka dhambi zote. Linafariji moyo wa huzuni, Latutia raha kuu. Katika shida na hatari kuu Yesu ni ngome yetu. Jina hilo katika giza huku hung'aa kama Nyota. Latuliza dhoruba na mawimbi Katika moyo wangu. Majina yote yasahauliwa, Ila jina la Yesu Milele litang'aa huko juu. Yesu jina zuri mno!

300. BWANA MUNGU NASHANGAA

Bwana Mungu nashangaa kabisa, Nikifikiri jinsi vilivyo, Nyota  ngurumo, Vitu vyote pia viumbwavyo kwa uwezo wako. Roho yangu na ikuimbie, Jinsi wewe ulivyo mkuu. Roho yangu na ikuimbie, Jinsi wewe ulivyo Mkuu. Nikitembea pote duniani, Ndege huimba nawasikia. Milima hupendeza macho sana, Upepo nao wafurahia.