278. NINAINUA MACHO YANGU.


Ninainua macho yangu Kwa Mungu aketiye juu,

Aliye msaada wangu, Njiani mwangu ni nuru,

Aliyefanya yote, Husikia maombi. Katika njia

Yangu yote Anilinda vema kweli.


Bwana hataniacha kamwe miguu yangu iteleze,

Yeye ndiye Mlinzi mwema, Ambaye hatasinzia.

Alinda roho yangu, Nisije kupotea, Baraka zake

Zinatosha, Kwa hitaji zangu zote.


Aniokoa na uovu, Aniponya roho yangu. Yeye

ni nguvu na wokovu, Ninahakikisha kweli.

Ananilinda pote, Kutoka na kuingia. Anijalia

mema yote, Nikimtumainia.

Comments

Popular posts from this blog

264. TWENDENI, WAKRISTO

267. BABA NAKUOMBA

263. ENYI KANISA LA MUNGU