277. NITAKAPOTOKA DUNIANI

 

Nitakapotoka duniani, Na kusimama mbele za Mungu,

Nitamwona Mkombozi wangu, Itakuwa utukufu kweli.


Itakuwa utukufu, utukufu, utukufu,

Kumwona Yesu Mwokozi wangu. Itakuwa utukufu kweli.


Huko mbinguni nitakapokaa, Pamoja nao watakatifu,

Nitamshukuru Mwokozi wangu, Itakuwa utukufu kweli.


Nitawaona wenzangu wote, Waliozishinda dhambi zote.

Na nitamwona Mwokozi wangu, Itakuwa utukufu kweli.


Je, ndugu umejitayarisha Kumwona Yesu Mwokozi wako,

Ili na wewe ushangilie, Na kuona utukufu kweli?

Comments

Popular posts from this blog

264. TWENDENI, WAKRISTO

267. BABA NAKUOMBA

263. ENYI KANISA LA MUNGU