288. TUNAMTIA MIKONONI MWAKO
Tunamtia mikononi mwako Mtoto huyu ili,
Atunzwe, Na kila siku kwa neema yako,
Bwana Yesu Kristo, umbariki!
Ulimwengu kuna majaribu, mahali
Pote kuna mitego, Lakini uwe Mchungaji
wake, Na umwongoze, Ee Rafiki Mwema.
Yesu umhifadhi kwa upendo, Asije
Akashindwa njiani, Na umlinde kwa
Rehema yako, Apate kuwa wako siku zote.
Utume nuru ya neema kwako, Na maji
Hai kutoka kwako, Ee Bwana Yesu
Twaku-omba leo: "Umlinde mwana wetu Salama!"
Comments
Post a Comment