290. BARAGUMU LITALIA SANA

 

Baragumu litalia sana, Watu wote Watalisikia.

Waliokufa watafufuka na Wazima watabadilika.

:/:Nani anayeweza? Yesu mwenyewe uwezo:/:


Na wenye uwezo wa duniani Watatetemeka  siku ile.

Na hawataweza kuinuka Kutazama uso kama jua.

:/: Nani anayeweza? Yesu mwenye uwezo:/:


Najua Mchunga wangu mwema, Anichunga Kwa maisha yangu,

 Na siku ile ya mwisho nikishinda, Sitaona uchungu wa kufa.

:/:Nani Mchunga mwema? Yesu Mwenye uwezo:/:


Mbinguni hakitafika kitu cha uchafu, Dhambi na kuasi.

Wasiomwamini Bwana Yesu Ghadhabu  ya Mungu yawangoja.

:/: Nani atahukumu? Yesu mwenye uwezo:/:


"Mimi Yesu mzabibu wa kweli, Baba Mungu Ndiye mkulima,

Na ninyi matawi ndani Yangu, Na hamwezi neno bila mimi."

:/: Nani ni mzabibu? Yesu mwenye uwezo.:/:


Unayempenda  Baba Mungu lazima Umpende ndugu yako,

Ukiwa hupendi ndugu yako, Huwezi kumpenda Baba Mungu.

:/: Nani aliyesema? Yesu Mwenye uwezo.:/:


"Nawapenda mwisho wa Upendo, Na ninyi Mpate kupendana,

Hivyo mataifa Wataona ya kwamba m-watu wangu kweli."

:/: Nani mwenye upendo? Yesu mwenye Uwezo.:/:


Sisi watumishi wake Mungu, Tu watu Maskini kati 'yote.

Tutakapowekwa pa Kuume, Kelele la sifa litashinda.

:/: Tutamsifu nani? Yesu, mwenye uwezo.:/:

Comments

Popular posts from this blog

264. TWENDENI, WAKRISTO

267. BABA NAKUOMBA

263. ENYI KANISA LA MUNGU