281. YOTE NINAYO NI KWA NEEMA


Yote ninayo ni kwa neema, Tangu

Nilipomwamini Bwana, Dhambi  na hatia

Zikafutwa, kwa neema yake nimeokoka.


Ameniokoa, Mwokozi Niliyekuwa mwenye

Dhambi, Niliyekufa nimefufuliwa, Kwa

neema yake nimeokoka!


Nilitawaliwa na Shetani, Kuelekezwa

Upotevuni, Bali Yesu akanitafuta,

Kwa neema yake nimeokoka.


Natakaswa na Yesu Mwokozi, Si kwa

Majuto wala machozi, Bali kwa damu

Nakombolewa, Kwa neema yake nimeokoka


Nimejaa shangwe na furaha, Na ninaimba

Nashangilia,  Kwa kuwa amenirehemia

Kwa neema yake nimeokoka.

Comments

Popular posts from this blog

264. TWENDENI, WAKRISTO

267. BABA NAKUOMBA

263. ENYI KANISA LA MUNGU