292. KATIKA DAMU
Katika damu safi ya Yesu Dhambi zangu Zilifutwa.
Katika mto ule wa afya Nalindwa na nguvu zake.
Nguvu za wokovu! Nguvu za ushindi!
Nazipata kisimani kinachojaa tele.
Nguvu za wokovu! Nguvu za ushindi
Damu inayonisafisha.
Kwa wingi wa neema ya Yesu Nimepona, Nimepona!
Wokovu ni kwa ajili yako, Na Kwa kila 'aminiye.
Nguvu zangu hazitoshi kweli, Ni dhaifu, Ni dhaifu,
Ila Yesu anifahamuye, Aniwezesha daima.
Baba yangu mwema anipenda, Anipenda, Anilinda!
Sitaogopa nguvu za mwovu, Yesu yu pamoja nami.
Comments
Post a Comment