291. MIMI MKOSAJI NILIKOMBOLEWA
Mimi mkosaji nilikombolewa, Alipojitoa Mwokozi.
Dhambi zangu zote Alizichukua, Kwa damu nilikombolewa.
Dhambi zilitungikwa msalabani, Alipojitoa Mwokozi.
Maumivu makuu! Walimdharau, Alipobeba dhambi zangu.
Yesu wa upole anihurumia, Ananitakasa Rohoni.
Nimesafishwa na nimewekwa Huru toka laana ya torati.
Naambatana na Yesu, siondoki, Kwa Kuwa alinificha.
Yesu, nakusifu Uliyepenipenda, Ukachukua dhambi zangu.
Comments
Post a Comment