274. NAFURAHIA KISIMA DAIMA


Nafurahia kisima daima Cha damu ya Yesu Kristo

Katika upendo nalindwa vema, Namsifu Yesu mpendwa.


Chemchemi hiyo inabubujika, Yaniletea uzima

Kando ya maji ninaburudika, Nashangilia daima.


Nakaa karibu na kisima hiki, Naishi kwa maji yake.

Yaniletea  kupita kipimo, Uzima na shangwe kweli.


Nakaa karibu na kisima hiki, Naishi salama sana.

Fika upesi uliye na kiu, Kisima chabubujika!


Nakaa karibu na kisima hiki, Ni furaha na uheri.

Na kando ya maji nafasi ipo, Waweza kupona kweli.

Comments

Popular posts from this blog

264. TWENDENI, WAKRISTO

267. BABA NAKUOMBA

263. ENYI KANISA LA MUNGU