271. NINASHIKWA NA KIU
Ninashikwa na kiu, Bwana, unipe maji,
maji ya uhai ndani ya maisha yangu.
:/: Bwana, Bwana Yesu Mfalme wangu!:/:
Moyo wangu wakupenda, Bwana Mungu wangu.
Nitakuja lini kwako, Bwana Mfalme wangu?
Mchana na usiku Bwana nakulilia. Watu
Wasema "Mungu wako yuko wap?"
Huzuni moyoni mwangu, Bwana Mungu wangu.
Watu wengi wadharau, Mungu 'wasamehe!
Twashikakama pamoja kwenda juu mbinguni.
Twashukuru, twafurahi kushirikiana.
Mwokozi, nguvu zaishaje moyoni mwangu?
Unisaidie Bwana, nitakushukuru.
Comments
Post a Comment