Posts

262. BADO KITAMBO

Bado kitambo - vita itakwisha, Kitambo Na dhoruba zapoa. Na tena nitalaza kichwa changu Mbavuni mwake Anipendaye. :/:Mbinguni hazitakuwamo Dhambi, Nitaziona raha na amani.:/: Bado kitambo - roho ya umizwa, Kitambo, Kati' usiku huu. Machozi ninatoa mara Nyingi, Maana bado sijamwona Yesu. :/: Lakini asubuhi ya milele, Huko Mbinguni sitalia tena.:/: Bado kitambo cha uchovu huku, Kitambo na nitamwona Yesu, Na huru Mbali ya hatari zote, Nastarehe mikononi mwake. :/: Uvuli wote utaondolewa, Kwa Nuru huko kamilifu kweli.:/: Mateso yangu hayadhuru tena, Nitayasahau kwake Yesu, Nikisumbuka Hapa duniani, Mbinguni nitastarehe  Kweli. :/: Na Mungu atafuta kila chozi, Ataondoa maumivu yote.:/:

263. ENYI KANISA LA MUNGU

Enyi kanisa la Mungu Punde vumilieni! Kati' nchi ya milele, Mtaona amani. :/: Kitambo kidogo, Na vita itakwisha.:/: Usilogwe na dunia, Usiache wokovu! Katika shida na raha, Umfuate Yesu tu! :/: Daima, daima, Utashida ubaya.:/: Ukichoka safarini, Njia ikiwa ndefu, Kwa hatari za jangwani, Mungu atakulinda. :/: Raha ya mbinguni, Yamtuliza msafiri!:/: Kwa imani tutaona Nchi yetu ya raha, Ni habari nzuri sana: Majaribu yakoma. :/:Twendeni, twendeni, Tukutane mbinguni!:/: Tukifariki dunia, Kwa furaha twaenda, Tulivyovitumaini, Ng'ambo tutaviona. :/: Furaha, furaha, Furaha ya milele.:/:

264. TWENDENI, WAKRISTO

Twendeni Wakristo wam-pendao Yesu, Tumwimbie na furaha, Tumwimbie  na furaha Kitini kwa Mungu, kitini kwa Mungu. Twendeni  mbinguni sisi tuliookoka, Twendeni tukatazame fahari ya Bwana wetu. Hawatafurahi wasiomjua Yesu, Bali tuokolewao, bali tuokolewao, Tum-sifu pote, tum-sifu pote. Tuna mibaraka yake, Mwokozi tele, Kabla hatujafikia, kabla hatujafikia Mji  wake Mungu, mji wake Mungu. Kwa hiyo twendeni furaha izidi, Tuache huzuni zote, tuache huzuni zote, Tufike kwa Yesu, tufike kwa Yesu.

265. TU WASAFIRI

Tu wasafiri, twakaribia Nchi ya Mbingukwa Mungu, Tusiogope bonde la kifo, Yesu anatuongoza. :/: Tu wasafiri :/: Tutakutana kwa Baba Mungu, Ee Bwana Yesu, utuongoze, Tufike sote Mbinguni. Wengi katika wapendwa wetu, Wamevuka mto wa kifo. Walifuata wito wa Mungu, Wakahamia huko juu. Katika mwendo wa duniani, Walimtazama Mwokozi. Na waliacha mambo ya huku, Walimpendeza  Yesu. Ndugu wapendwa, tuendelee, hata Tukiwa na shida! Yesu ni njia, kweli, Uzima, Tumfuate daima!

266. NATAKA NIMJUE YESU

Nataka nimjue Yesu, Na nizidi kumfahamu, Nijue pendo lake na Wokovu wake kamili. Zaidi, zaidi, nimfahamu Yesu, Nijue pendo lake na Wokovu wake kamili. Nataka nione Yesu, Na nizidi kusikia, Anenapo kitabuni, Kujidhihirisha kwangu. Nataka nifahamu na, Nizidi kupambanua, Mapenzi yake nifanye, Yale yanayompendeza. Nataka nikae naye, Kwa mazungumzo zaidi, Nizidi kuwaonyesha, Wengine wokovu wake.

267. BABA NAKUOMBA

Baba, nakuomba asubuhi hii, Niongoze kweli katika yote. Ee, Baba sikia Maombi yangu. Nakusifu Baba, Wanisikia. Ninapoifanya kazi ya leo, Unitie nguvu, naomba Bwana. Mchana uishapo, usiku waja, Baba unilinde, ninakuomba. Maadui wengi wananiwinda, Maishani mwangu. Mungu 'nilinde! Siku zangu zote ulimwenguni, Niwe na amani, hadi mwishoni.

268. EE YESU INGIA ROHONI

  Ee Yesu ingia rohoni mwangu, Ili nitakaswe Niwekwe huru, Nipate kushirikiana  nawe, Katika mateso na raha yako. Nifahamishe uwezo wako!  Nisulubishwe pamoja nawe! Nifahamishe  uwezo wako! Nisulubishwe pamoja nawe! Siombi ufalme, siombi sifa, Naomba neema Yako daima, Nijue yakini ya msalaba, Ulipokufa Kwa ajili yangu. Ingia rohoni, unichunguze, Unisaidie katika Yote, Kusudi nipate nia moyoni, Nijitoe kweli Kwako Mwokozi. Hakuna neno la kunizuia, Kuwa na umoja Nawe Mwokozi, Nitawezaje kufika mbinguni, Nisipounganishwa naye Yesu?