295. SHANGILIENI EE WATU WA MUNGU


Shangilieni Ee watu wa Mungu! Yesu

Bwana alitumwa kwetu. Neema kubwa,

Pendo la ajabu tum-sifu Mungu siku zote!


Mungu wetu mwenye mamlaka yote

U ngao na kimbilio letu, Unayasikia

maombi yetu, jina lako litukuzwe!


Shangilieni Ee watu wa Mungu!

Tumwimbie nyimbo za furaha! Tusiogope

Bali tumwamini, Twende mbele kwa uwezo Wake!


Shangilieni Ee watu wa Mungu!

Tumeokoka kutoka dhambi. Jirani zetu

Wasioamini, tuwaongoze wamjue Yesu!


Shangilieni Ee watu wa Mungu! Mfalme

Wetu yuaja tena! Kitambo kidogo tutaingia

Mbinguni kwake Mwokozi wetu!

Comments

Popular posts from this blog

264. TWENDENI, WAKRISTO

267. BABA NAKUOMBA

263. ENYI KANISA LA MUNGU