273. NI UHERI KUMWAMINI MUNGU
Ni uheri kumwamini Mungu, Kama Ibrahimu zamani.
Hakutiwa shaka kwa uchungu, Ila alitiii kwa imani.
Ni uheri kuendea sawa, Katika mapito ya kweli.
Ukijaribiwa na kukawa, Mwisho wake utajaliwa.
Mashujaa wote wa Biblia, Hawakufuata anasa.
Wakafunzwa kum-tegemea, Mungu Baba mwenye uweza
Nao wakaenda kwa imani, Ya kutetemesha dunia
Wkashida giza na shetani, Sifa na heshima kwa Mungu.
Yeye atakayekuzwa naye Kwanza, atajinyenyekeza.
Baba anayempenda Mwana, Anamrudi kwa upendo.
Hivyo Mungu anawakamilisha watu wake wanapoteswa.
Na zaidi kuwafahamisha kulijua pendo lake kuu.
Na ikiwa raha ya dunia yatoweka kwa majaribu.
Mwaminifu atamfurahia Mungu kwani yupo karibu.
Na mavuno ya taabu yake Yakitekelezwa motoni,
Atamgemea Bwana wake, Kwa hiyo hatanung'unika.
Jipe moyo enyi kundi dogo msiogope hatarini.
Shika neno la Mwenyezi Mungu liwaongoze safarini.
Haleluya kwani majaribu yanahimiza msafiri.
Naye ataona kwa karibu Mji wa amani Mbinguni.
Comments
Post a Comment