276. EE MUNGU MWENYEZI


Ee Mungu Mwenyezi, matendo yako Yapita fahamu zote,

lakini hakika najua kwamba, Njia yako ndiyo bora.


"Mtoto wangu huwezi kujua, Jinsi nikutendeavyo.

Lakini usiogope mwanangu, Mateso yote 'takwisha."


Ee Bwana, unayo magari mengi Na lile linalonifaa,

Unichagulie mwenyewe, Bwana, Nifike salama kwako!


Na kama nitaondoka haraka, Kama Eliya zamani,

Uchungu na shida zote 'takwisha, Nitakwenda kwa amani.


Tutamsujudia Yesu pamoja, Na watakatifu wote.

Mungu mwenye haki hata milele, Katika matendo yake.


Nangoja kwa uvumilivu sasa, Kuchukuliwa na wewe.

Natarajia uzima milele, Uridhi wangu mbinguni.

Comments

Popular posts from this blog

264. TWENDENI, WAKRISTO

267. BABA NAKUOMBA

263. ENYI KANISA LA MUNGU