265. TU WASAFIRI


Tu wasafiri, twakaribia Nchi ya Mbingukwa Mungu,

Tusiogope bonde la kifo, Yesu anatuongoza.


:/: Tu wasafiri :/: Tutakutana kwa Baba Mungu,

Ee Bwana Yesu, utuongoze, Tufike sote Mbinguni.


Wengi katika wapendwa wetu, Wamevuka mto wa kifo.

Walifuata wito wa Mungu, Wakahamia huko juu.


Katika mwendo wa duniani, Walimtazama Mwokozi.

Na waliacha mambo ya huku, Walimpendeza  Yesu.


Ndugu wapendwa, tuendelee, hata Tukiwa na shida!

Yesu ni njia, kweli, Uzima, Tumfuate daima!


Comments

Popular posts from this blog

264. TWENDENI, WAKRISTO

267. BABA NAKUOMBA

263. ENYI KANISA LA MUNGU