263. ENYI KANISA LA MUNGU
Enyi kanisa la Mungu Punde vumilieni!
Kati' nchi ya milele, Mtaona amani.
:/: Kitambo kidogo, Na vita itakwisha.:/:
Usilogwe na dunia, Usiache wokovu!
Katika shida na raha, Umfuate Yesu tu!
:/: Daima, daima, Utashida ubaya.:/:
Ukichoka safarini, Njia ikiwa ndefu,
Kwa hatari za jangwani, Mungu atakulinda.
:/: Raha ya mbinguni, Yamtuliza msafiri!:/:
Kwa imani tutaona Nchi yetu ya raha,
Ni habari nzuri sana: Majaribu yakoma.
:/:Twendeni, twendeni, Tukutane mbinguni!:/:
Tukifariki dunia, Kwa furaha twaenda,
Tulivyovitumaini, Ng'ambo tutaviona.
:/: Furaha, furaha, Furaha ya milele.:/:
Comments
Post a Comment