272. NI SIKU TUKUFU


Ni siku tukufu, haleluya amina,

Ya kupum-zika, haleluya, amina.

Tuache shughuli tumwabudu Mungu,

Bwana wa mbinguni, haleluya amina.


Ni siku tukufu, haleluya amina,

Tukufu kabisa, haleluya, amina.

Njoni ndugu zangu, tumwabudu Mungu,

Kwa roho na kweli, haleluya, amina.


Ni siku tukufu, haleluya, amina,

Ya furaha mno, haleluya, amina.

Yesu 'kafufuka, na sasa yu hai,

Anatuombea, haleluya, amina.


Ni siku tukufu, haleluya, amina,

Ndiyo maarufu, haleluya, amina.

Tunaye Mwokozi atuokoaye,

Sasa na milele haleluya, amina.


Ni siku tukufu, haleluya, amina,

Siku ya neema, haleluya, amina.

Tangazeni Neno la Bwana Mwokozi,

Msifuni daima, haleluya, amina.

Comments

Popular posts from this blog

264. TWENDENI, WAKRISTO

267. BABA NAKUOMBA

263. ENYI KANISA LA MUNGU