294. UTUME ROHO WAKO


Utume roho wako juu yetu Kama kwa

Siku ya Pentekoste. :/: Uwashe moto wako

Ndani yetu, Tusiwe wenye uvuguvugu.:/:


Utume Roho wako juu yetu Kama

Ulivyofanya zamani, :/: Mtume Petro

Alihubiri katika nyumba ya Kornelio,:/:


Utume Roho wako juu yetu, Tupewe nasi

Uwezo wako.:/: Maelfu wenye dhambi

Waokoke na Neno lako tulieneze.:/:


Utume Roho wako juu yetu, Nyosha

Mkono wako wa nguvu, :/: Ishara na ajabu

Zifanyike wagonjwa waponywe kati yetu.:/:


Uwaamshe waliosinzia, Waliodhoofika

Safarini. :/: Ee Bwana, utujie kama kale

Ulipowapa watu Baraka.

Comments

Popular posts from this blog

264. TWENDENI, WAKRISTO

267. BABA NAKUOMBA

263. ENYI KANISA LA MUNGU