296. DHAMBI ZANGU ZIMEONDOLEWA
Dhambi zangu zimeondolewa, Mambo ya
Giza nimeyaacha. Yesu Kristo amenisafisha,
Ninamfurahia Mwokozi wangu.
Ninalo kao mbinguni Nami nimepewa vazi,
Thawabu ya ushindi ni Taji ya uzima.
Yesu ni Mwokozi wangu. Alinikomboa,
Alilipa deni langu Pendo lake kubwa nalisifu
daima, Ninamfurahisha Mkombozi.
Nimeokoka toka gizani, Zimekwisha siku
Za huzuni. Nikitapa raha na amani,
Wakati Yesu aliponikomboa.
Shaka na hofu zimeondoka, Na siogopi
Mauti tena. Yesu Kristo ni rafiki yangu.
Kwake ninalindwa vema siku zote.
Roho wa Mungu anijaliza, Ananifariji
Safarini. Yesu Kristo yu karibu nami,
Yeye ni ngao yangu na kimbilio.
Comments
Post a Comment