262. BADO KITAMBO


Bado kitambo - vita itakwisha, Kitambo Na dhoruba zapoa.

Na tena nitalaza kichwa changu Mbavuni mwake Anipendaye.

:/:Mbinguni hazitakuwamo Dhambi, Nitaziona raha na amani.:/:


Bado kitambo - roho ya umizwa, Kitambo, Kati' usiku huu.

Machozi ninatoa mara Nyingi, Maana bado sijamwona Yesu.

:/: Lakini asubuhi ya milele, Huko Mbinguni sitalia tena.:/:


Bado kitambo cha uchovu huku, Kitambo na nitamwona Yesu,

Na huru Mbali ya hatari zote, Nastarehe mikononi mwake.

:/: Uvuli wote utaondolewa, Kwa Nuru huko kamilifu kweli.:/:


Mateso yangu hayadhuru tena, Nitayasahau kwake Yesu,

Nikisumbuka Hapa duniani, Mbinguni nitastarehe  Kweli.

:/: Na Mungu atafuta kila chozi, Ataondoa maumivu yote.:/:


Comments

Popular posts from this blog

264. TWENDENI, WAKRISTO

267. BABA NAKUOMBA

263. ENYI KANISA LA MUNGU