299. UNAJUA JINA TULILOPEWA


Unajua jina tulilopewa tuokolewa kwalo?

Linasifiwa duniani pote katika watu wote.

Yesu ndilo jina lipitalo Kila jina duniani!

Ni lenye nguvu ya kutuokoa kutoka dhambi zote.


Linafariji moyo wa huzuni, Latutia raha kuu.

Katika shida na hatari kuu Yesu ni ngome yetu.


Jina hilo katika giza huku hung'aa kama Nyota.

Latuliza dhoruba na mawimbi Katika moyo wangu.


Majina yote yasahauliwa, Ila jina la Yesu

Milele litang'aa huko juu. Yesu jina zuri mno!

Comments

Popular posts from this blog

264. TWENDENI, WAKRISTO

267. BABA NAKUOMBA

263. ENYI KANISA LA MUNGU