289. NINATAMANI KWENDA.


Ninatamani kwenda mbinguni nchi yangu,

Niliyepewa na Mungu kwa imani. Ni

Shangwe bora kuona mji ule, Kwa

Kwenda kule sitaogopa kitu.


Ee Baba yangu niongoze, unisafishe  kwa

damu ya Mwokozi! Nifananishe na

theluji, Unibatize kwa Roho Mtakatifu!


Ee Mungu tumepata Mwana Yesu Kristo.

Kipawa kweli kinachoshinda yote.

Anahubiri amani kwao wote, walio huku

Kribu, nao mbali.


Kwa Yesu tumepata mwisho wa upendo

Na njia ya kumwendea Baba Mungu. Si

Wapitaji na tena si wageni, Tunatumika

Kwa roho ya upendo.


Amani kwetu na matumaini tele, Salamu

Toka kwa Mungu wa milele. Ni posho ya

Watumishi wa upendo Tutaurithi uzima

Wa milele.

Comments

Popular posts from this blog

264. TWENDENI, WAKRISTO

267. BABA NAKUOMBA

263. ENYI KANISA LA MUNGU