284. TUMESOMA MENGI
Tumesoma mengi juu ya Bwana Yesu
Upendo wake, ishara zake. Na usome tena,
Ukamwombe Mungu, Na utaona maajabu.
Hata leo yanatokea, Tunapoomba kwa imani.
Tuombe tu, Atusikia, Na tuatona maajabu.
Jamaa ya Naini wakosa amani,
Wafadhaika, Wahuzunika. Bali Bwana
Yesu 'kafanya ajabu. Aliyekufa 'kahuika.
Ahadi ya Mungu, Roho mtakatifu,
Ilitimizwa Yerusalemu. Walikutanika,
Roho akashuka, Kwa lugha mpya wakamsifu.
Petro kahutubu, wengi wakatubu,
wakagairi Dhambi za siri, Waliopokea
Neno lake Bwana Wakabatizwa siku ile.
Nilimwomba Yesu, Nikapata nguvu,
Na jambo hili ni la fadhili, Nilisamehewa
Dhambi zikafutwa, Nimeupokea wokovu.
Comments
Post a Comment