275. EE MUNGU MWENYE HAKI
Ee Mungu mwenye haki, niongoze huku Katika
mambo yote yakupendezayo. Bila wewe,
Bwana Yesu, mashaka mengi ninayo Ya
kunitisha hapa safarini mwangu.
Kumtegemea Yesu ni heri daima, na kutembea
naye kwa kila hatua, Kwa kuwa yeye ni
Mchunga. Ananiongoza vema, Nipate kuingia
kwake mbinguni juu.
Nina safari sasa ya kwenda mbinguni.
Mwokozi yuko huko, Lazima nifike. Na siku ya
kuingia Nitashangilia kweli Kumwona na kum-sifu
Mwokozi wangu.
Ulimwenguni huku kuna shida nyingi,
Nikihitaji kitu, ninahangaika. Lakini siku ile kuu
nitakapomwona Yesu, Natumiani sitaikosa Thawabu.
Mbinguni sitaona uovu wowote. Wala kukuta
Mambo ya huzuni tena. Sauti nitamtolea
kusema: "Ee, Mungu mwema!" Mikono
nitaipepea kwa shangwe kuu.
Comments
Post a Comment