268. EE YESU INGIA ROHONI

 

Ee Yesu ingia rohoni mwangu, Ili nitakaswe

Niwekwe huru, Nipate kushirikiana  nawe,

Katika mateso na raha yako.


Nifahamishe uwezo wako!  Nisulubishwe

pamoja nawe! Nifahamishe  uwezo wako!

Nisulubishwe pamoja nawe!


Siombi ufalme, siombi sifa, Naomba neema

Yako daima, Nijue yakini ya msalaba, Ulipokufa

Kwa ajili yangu.


Ingia rohoni, unichunguze, Unisaidie katika

Yote, Kusudi nipate nia moyoni, Nijitoe kweli

Kwako Mwokozi.


Hakuna neno la kunizuia, Kuwa na umoja

Nawe Mwokozi, Nitawezaje kufika mbinguni,

Nisipounganishwa naye Yesu?


Comments

Popular posts from this blog

264. TWENDENI, WAKRISTO

267. BABA NAKUOMBA

263. ENYI KANISA LA MUNGU