283. NIMEYASIKIA MENGI


Nimeyasikia mengi aliyofanya Yesu

Alipokuwa hapa duniani. Pote alienda

mema, aliwasaidia. Kwa furaha ninaimba:

"Yesu ni yeye Yule."


Yesu ni Yeye  Yule Jana leo, daima!

Hutafuta wakosa, Huokoa waovu.

Mwokozi ni yeye Yule


Ni kipofu yule, Jina lake ni Bartimayo,

Aliposikia Yesu apita, Kwa imani akaomba

Akaponywa na Yesu. Nafurahi kwa kuimba:

"Yesu ni yeye Yule".


Wenye dhambi na wagonjwa na maskini waitwa

kwa Yesu, Mwokozi mwenye rehema. Uiguse

nguo yake, sawa na mama yule, Utapewa nguvu

zake, Yesu ni yeye Yule!


Najisikia jinsi alivyowaombea Maadui wake

msalabani. Aliteswa kwa miiba, aliona uchungu.

Kwa furaha ninaimba: "Yesu ni yeye Yule".

Comments

Popular posts from this blog

264. TWENDENI, WAKRISTO

267. BABA NAKUOMBA

263. ENYI KANISA LA MUNGU